Iran: Tuko tayari kurejea kwenye mazungumzo ya 'haki'
29 Agosti 2025Katika barua yake aliyomuandikia mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas, Araqchi amesisitiza utayari na nia thabiti ya Iran kuanza tena mazungumzo ya kidiplomasia ya haki na yenye uwiano, kwa sharti kwamba pande nyingine zionyeshe umakini na nia njema na kuepuka vitendo vinavyohatarisha uwezekano wa kufikia makubaliano.
Araqchi ameyasema hayo saa chache baada ya Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kuanzisha mchakato wa siku 30 wa kuiwekea tena Iran vikwazo vya Umoja wa Mataifa, kutokana na mpango wake wa nyuklia
Aidha, Umoja wa Mataifa umeitolea wito Iran na mataifa hayo matatu yenye nguvu ya Ulaya kuongeza kasi katika kuyafikia makubaliano ya nyuklia, ndani ya siku 30 zijazo, kabla ya kurudisha tena vikwazo hivyo vya Umoja wa Mataifa vilivyochochewa na Ulaya.