Iran iko tayari kujenga upya imani na madola ya Ulaya
18 Mei 2025Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi Abbas Araghchi ameuambia mkutano wa kidiplomasia mjini Tehran kuwa Iran iko tayari, kama itahisi kuna dhamira ya dhati na mtizamo huru kutoka kwa mataifa ya Ulaya, kuanzisha sura mpya katika mahusiano yake na Ulaya.
Ijumaa iliyopita, wanadiplomasia waandamizi wa Iran walikutana na maafisa wenzao kutoka Uingreza, Ufaransa na Ujerumani kwa mazungumzo kuhusu hali ya mazungumzo ya nyukliakati ya Marekani na Iran.
Tehran imefanya duru nne za mazungumzo ya nyuklia na Washington yakisimamiwa na Oman, yakiwa ndio ya ngazi ya juu kati ya mahasimu hao wawili tangu Marekani ilipojiondoa kwenye mkataba wa nyuklia wa 2015.
Madola hayo matatu yenye nguvu barani Ulaya -- ambayo ni sehemu ya mwafaka wa 2015, yanatafakari kama yataidhinisha kifungu cha kisheria ambacho kitarejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran. Kifungu hicho kinamalizika Oktoba mwaka huu.