Iran yasema haitokubali mkataba utakaoinyima haki
2 Juni 2025Iran imesema haitokubali kuingia kwenye mkataba wa Nyuklia ambao utainyima kile inachokiita haki ya kundesha shughuli zake za amani.
Kauli hiyo ya Iran inalenga kuonesha msimamo wake kuhusu suala la urutubishaji madini ya Urani, wakati ikiishinikiza Marekani, kuipatia hakikisho la kuiondolea vikwazo.
Suala hilo la urutubishaji Urani, limebakia kuwa kipengee cha msingi kwenye mvutano kati ya mataifa hayo mawili hasimu,kwenye mazungumzo ya kutafuta makubaliano yaliyoanza mwezi Aprili.
Waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Aragchiakiwa mjini Cairo ambako amekutana na mkuu wa shirika la kimataifa la kudhibiti matumizi ya nguvu za Atomiki,Rafael Grossi, amesema nchi yake haiwezi kufikia makubaliano yoyote ikiwa itazuiwa kuendesha mradi wake wa matumizi ya kiraia.
Grossi ameitaka Iran kuwa na uwazi katika suala la urutubishaji Urani baada ya ripoti kuonesha nchi hiyo imeongeza kiwango cha urutubishaji.