MigogoroIran
Iran, China na Urusi kuanza luteka za pamoja za kijeshi
11 Machi 2025Matangazo
Luteka hizi zilizopewa jina Ukanda wa Usalama wa Majini, na ambazo hufanyika kila mwaka zinaanza hii leo karibu na mji wa bandari wa Chabahar katika Ghuba ya Oman.
Shirika la habari la Tasnim lenye ushirika na serikali ya Iran limeripoti kwamba luteka hizo zinalenga kuimarisha usalama wa kikanda na kutanua ushirikiano baina ya mataifa hayo.
Ghuba ya Oman ina umuhimu wa kimkakati kwa ajili ya biashara ya kimataifa, inayofungua njia kuelekea Ujia wa Hormuz ambao ni njia muhimu kwa ajili ya usafirishaji wa mafuta.