Iran: Balozi wa Ujerumani akutana na mpinzani wa serikali:
1 Februari 2004Matangazo
TEHERAN: Balozi wa Ujerumani nchini Iran amekuwa ni mwanadiplomasia wa kwanza wa nchi ya Magharibi kukutana na mhakiki wa serikali ya Teheran Ayatollah Hussein-Ali Montaseri. Mkutano huo kati ya balozi Paul Freiherr von Maltzahn na Ayatollah Montaseri ulifanyika tayari Jumatatu iliyopita katika mji wa Ghom, lakini ulitangazwa sasa tu, liliarifu shirika la habari la Ujerumani. DPA. Kwa muda wa miaka mitano Ayatollah Montaseri alipewa kifungo cha nyumbani. Hapo mwaka 1989, kiongozi wa zamani wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Khomeini alipokonya Ayatollah Montaseri wadhifa wa kuwa mfuasi wake kufuatana na kulaumu kwake mfumo wa utawala wake wa Kiislamu nchini Iraq.