IPOA: Watu 65 waliuwawa katika maandamano Kenya
24 Julai 2025Matangazo
Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo leo Alhamisi imebaini ukiukaji mkubwa wa viwango vya kikatiba vya uendeshaji wa polisi ikiwa ni pamoja na matumizi ya nguvu kupita kiasi, ukosefu wa weledi, na kushindwa kulinda usalama wa umma na haki za raia.
IPOA pia imesema kuwa vurugu, uporaji na uharibifu wa mali uliofanywa na watu waliovaa kama waandamanaji au magenge ya kihuni waliotumia fursa, ulikuwa wa aina yake na mara nyingine uliwazidi nguvu polisi.
Hata hivyo rais William Ruto ameendelea kuwatetea polisi na hatua zao, huku akinukuliwa akitoa amri ya waandamanaji wanaofanya vurugu wapigwe risasi mguuni.