JamiiMyanmar
IOM: Biashara haramu ya binaadamu yaongezeka kwa kasi kubwa
31 Julai 2025Matangazo
Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM limesema katika Siku ya Kimataifa ya Kupinga Usafirishaji Haramu wa Binadamu kwamba waathiriwa mara nyingi hawapati msaada na badala yake hukamatwa kwa uhalifu ambao hawakuufanya.
Mkurugenzi wa IOM Amy Pope amesema usafirishaji haramu wa binadamu sio tu ni mzozo wa haki za binadamu, bali pia ni biashara kubwa ya kimataifa inayochochea ufisadi na kueneza hofu.
Amesema biashara hiyo ambayo huleta wastani wa dola bilioni 40 kwa mwaka, huwanasa zaidi wahamiaji, vijana wanaotafuta kazi, watoto na watu wenye ulemavu.
Ameziomba serikali na mashirika ya kiraia kushinikiza mabadiliko ya sheria za kitaifa ili waathirika wa usafirishaji haramu wa binadamu walindwe badala ya kuadhibiwa.