SiasaIndonesia
Indonesia na Marekani waanza luteka za pamoja za mwaka
25 Agosti 2025Matangazo
Luteka hizo, zinazolenga kuhakikisha uthabiti katika eneo la Asia-Pasifiki, zinafanyika wakati Marekani inaangazia kuhakikisha washirika wao wanachukulia kwa uzito zaidi vitisho ambavyo huenda vikaletwa na China.
Zaidi ya wanajeshi 4,000 wa Indonesia na 1,300 wa Marekani wanashiriki luteka hizo za hadi Septemba 4, sambamba na wanajeshi kutoka Australia, Japan, Ufaransa, Uingereza na kwingineko.
Luteka za mwaka huu za "Super Garuda Shield" ni kubwa zaidi kuwahi kufanyika tangu zilipoanza mwaka wa 2009, na zinafanyika katika mji mkuu, Jakarta, pamoja na maeneo ya kisiwa cha Sumatra na visiwa vya Riau.