SiasaIndia
India yasema itaendelea kununua mafuta kutoka Urusi
2 Agosti 2025Matangazo
Maafisa wawili wa serikali ya India ambao hawakutaka kutajwa majina yao kutokana na unyeti wa suala hilo wamesema India ina mikataba ya muda mrefu na Urusi na kwamba si rahisi kuacha mara moja kununua mafuta kutoka Urusi.
Wizara ya Mambo ya Nje ya India imesisitiza uhuru wa kujiamulia yenyewe juu ya masoko ya nishati.
Rais Trump ametishia kuwatoza ushuru wanaonunua mafuta ya Urusi na ametishia kuzitoza ushuru wa hadi asilimia mia moja, nchi zinazoagiza mafuta kutoka Urusi ikiwa nchi hiyo haitafikia mapatano ya amani na Ukraine. India inakidhi asilimia 35 ya mahitaji yake ya mafuta kutoka Urusi.