MigogoroAsia
India yasema haina nia ya kuuzidisha mzozo wake na Pakistan
8 Mei 2025Matangazo
Waziri Jaishankar amesema nchi yake haina nia ya kuuzidisha mzozo huo lakini ameonya kuwa watajibu vikali mashambulizi yoyote:
" Majibu yetu yalilenga maeneo rasmi na yalipimwa. Si nia yetu kuzidisha hali hii ya mvutano. Lakini, iwapo kuna mashambulizi ya kijeshi dhidi yetu, pasiwe na shaka kwamba yatakabiliwa na majibu madhubuti. Kama jirani na mshirika wa karibu, ni muhimu kuwa na uelewa mzuri wa hali hiyo."
Pakistan imesema hii leo kuwa ilidungua droni 25 zililizorushwa na India na kulazimika kuvifunga viwanja vyake vya ndege katika miji ya Lahore, Islamabad na Karachi. Mashirika ya ndege nchini India yamesitisha pia za safari za ndege kwenye viwanja vya zaidi ya 10 katika mikoa ya kaskazini na magharibi kufuatia mvutano huo na Pakistan.