MigogoroAsia
India yaishambulia Pakistan kwa makombora
7 Mei 2025Matangazo
Mamlaka za Pakistan zimesema makombora ya India yalililenga jimbo linalozozaniwa na pande hizo mbili la Kashmir pamoja na mkoa wa mashariki wa Punjab. Moja ya makombora liliupiga msikiti kwenye mji wa Bahawalpur na kusababisha kifo cha mtoto mmoja na kujeruhiwa watu wengine kadhaa.
Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif amelaani mashambulizi hayo ya anga na kusema nchi yake inayo haki ya kulipa kisasi kwa hujuma hizo za India alizozitaja kuwa "kitendo cha kivita".
Mvutano kati ya mataifa hayo mawili umezidi makali mnamo wiki za karibuni, tangu India ilipoilaumu Pakistan kwa shambulizi la wanamgambo lililotokea mwezi uliopita jimboni Kashmir.
India inasema Pakistan inawaunga mkono wale waliotenda tukio hilo lililosababisha vifo vya watu 26.