AfyaIndia
India yachunguza ugonjwa usiojulikana ulioua watu 17
25 Januari 2025Matangazo
Vifo hivyo vilitokea tangu Desemba mwaka jana katika kijiji cha Badhaal katika eneo la Jammu huko Rajouri. Ugonjwa huo usiojulikana unaharibu kwa kiasi kikubwa mishipa ya ubongo hadi kusababisha kifo.
Mapema wiki hii, hali ya dharura ya kiafya ilitangazwa katika kijiji hicho, huku takriban watu 230 wakiwekwa karantini. Serikali ya shirikisho imeanzisha uchunguzi wa kina huku waziri wa afya Jitendra Singh akisema kuwa uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa vifo hivyo "havikutokana na maambukizi yoyote, virusi au bakteria bali aina fulani ya sumu.