MigogoroAsia
India yawaua magaidi waliohusika na shambulio la Kashmir
29 Julai 2025Matangazo
India inawataja washambuliaji hao waliowauwa watalii 26 kuwa ni raia wa Pakistan walioungwa mkono na serikali ya Islamabad. Katika shambulio hiyo watu hao waliwafyatulia risasi watalii walipokuwa katika eneo lenye milima na mandhari ya kuvutia la Pahalgam kabla ya kutokoma msituni. Mauaji hayo yalichochea mzozo mbaya wa kijeshi wa siku nne kati ya India na Pakistan.Pakistan yenyewe inakanusha kuwa haikuhusika na tukio hilo.