Ripoti za utafiti wa kisayansi zimeafiki kuwa saratani za shingo ya kizazi hutokana na maambukizi ya virusi vya 'Human Papillomavirus' au HPV vilivyoko katika jamii ya papilloma. Kwa mujibu wa WHO ulimwenguni kote saratani ya shingo ya kizazi ni saratani ya nne kwa kuathiri wanawake.