Idadi ya watu waliofariki kwa moto huko Macedonia yafikia 59
16 Machi 2025Serikali ya Macedonia imesema hii leo kwamba idadi ya watu waliofariki kutokana na moto uliotokea katika klabu ya usiku imefikia watu 59, huku 35 kati yao wakiwa tayari wametambuliwa.
Waziri wa Mambo ya ndani wa Macedonia Pance Toskovsk amesema katika taarifa kwamba zaidi ya watu 100 wamejeruhiwa katika ajali hiyo ya moto iliyotokea katika klabu ya usiku inayojulikana kama "Club Pulse" iliyopo katika mji wa mashariki wa Kocani.
Soma zaidi: Angola yatoa wito wa kusitisha mapigano mashariki mwa Kongo
Wizara hiyo imeongeza kuwa tayari imetoa waranti wa kukamatwa kwa watu wanne kufuatia mkasa huo. Inaelezwa kwamba klabu hiyo ya usiku ilikuwa na watu zaidi ya 1,000 wengi wao wakiwa vijana ambao walikuja kushuhudia wasanii wa muziki wa kufoka foka maarufu hip-hop waitwao DNK.