MigogoroMashariki ya Kati
Wapalestina waliouwawa Ukanda wa Gaza wafikia 56
26 Juni 2025Matangazo
Msemaji wa Idara hiyo Mahmud Bassal, amesema mauaji hayo yamefanywa katika maeneo kadhaa ndani ya ukanda huo. Miongoni mwa waliouawa ni watu sita waliokuwa wakisubiri msaada ya kiutu katika maeneo tofauti.
Soma zaidi: Israel yaendeleza mashambulizi Gaza
Wakati huohuo Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez amesema kinachoendelea Gaza ni mauaji ya halaiki. Sanchez ametoa wito kwa Umoja wa Ulaya kusitisha mara moja mkataba wake wa ushirikiano na Israel.
Mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza ya kulipa kisasi dhidi ya kundi la Hamas lililowauwa watu 1,219 mnamo Oktoba 7, 2023 hadi sasa yameshasababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina 56,000 kwa mujibu wa Wizara ya afya ya Gaza iliyo chini ya kundi la Hamas.