WHO:Waliouwawa Sudan katika shambulio hospitalini wafikia 70
26 Januari 2025Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, Gebreyesus amesema wakati wa shambulio katika hospitali hiyo pekee inayotoa huduma kwenye mji wa El Fasher, kulikuwa na wagonjwa waliokuwa wapatiwa huduma.
Mkuu huyo wa Shirika la Afya duniani ametoa wito wa kusitishwa kwamashambulizi dhidi ya vituo vya huduma ya afya na wafanyakazi wake nchini Sudan na kuruhusu kutengenezwa kwa vifaa vilivyoharibiwa katika shambulio hilo.
Soma zaidi:Mashambulizi ya siku mbili ya RSF huko El-Fasher yaua watu 48
Awali, akielezea shambulio hilo, Gavana wa Darfur Mini Minnawi kupitia ukurasa wake wa X amesema droni ilishambulia kitengo cha dharura cha hospitali hiyo na kuwauwa wagonjwa wakiwemo wanawake na watoto. Mapigano makali, yanaendelea katika mji wa El Fasher kati ya kundi la wapiganaji wa RSF na muungano wa vikosi vya jeshi la Sudan likiwemo jeshi lenyewe, pilisi, makundi ya waasi na vikosi vya ulinzi vya eneo hilo.