Watu wanane wauawa Ukraine kufuatia mashambulizi ya Urusi
1 Februari 2025Wizara ya mambo ya ndani ya Ukraine imesema kombora moja liliangukia katika nyumba na kuwauwa watu wanne huko Poltava. Watu 13 walijeruhiwa kwenye eneo hilo wakiwemo watoto watatu.
Mtu mmoja ameuwawa katika mji wa Kharkiv na wanne wamejeruhiwa kutokana na shambulio la droni. Mamlaka za mkoa wa Summy wamebainisha kuwa maafisa watatu wa polisi waliuwawa wakati wa mashambulizi katika kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa mkoa huo.
Makazi kadhaa ya watu pamoja na miundombinu ya umeme nayo imeharibiwa wakati wa mashambulizi hayo. Majengo 18 ya makazi ya raia, shule ya checkechea na miundo mbinu ya umeme katika mji wa Poltava viliharibiwa katika mashambulizi hayo ya Urusi.
Kulingana na jeshi la anga la Ukraine, Urusi ilirusha makombora 165 na droni katika mashambulizi hayo ya usiku wa kuamkia Jumamosi.