JangaNigeria
Idadi ya waliokufa kwa mafuriko Nigeria yapindukia 151
31 Mei 2025Matangazo
Hayo yameelezwa na Rais wa nchi hiyo Bola Tinubu ambaye pia ametahadharisha kuwa idadi ya vifo huenda ikaongezeka.
Mvua kubwa za masika zilizoanza siku ya Jumatano na kuendelea kunyesha hadi Alhamisi wiki hii zimeleta balaa la mafuriko yaliyosomba na kuzamisha nyumbva katika mwa Nigeria.
Mji mdogo wa Mokwa ulio karibu na Mto Niger ndiyo umeshuhudia athari kubwa zaidi ambapo miili ya watu imebebwa na maji kufuata mkondo wa mto huo hali inayofanya kuwa vigumu kuipata kwa uharaka.
Rais Tinubu amesema vikosi vya usalama vimetumwa kuwasaidia watoa huduma za dharura na msaada mwingine kama maakazi ya muda na mahitaji muhimu vinasambazwa.