Idadi ya waliokufa kwa mafuriko Marekani yafikia 78
7 Julai 2025Matangazo
Idadi ya watu waliopoteza maisha kufuatia mafuriko makubwa yaliyoyakumba maeneo ya kati mwa jimbo la Texas, Marekani, imefikia watu 78, wakiwemo watoto 28. Taarifa hiyo imetolewa na maafisa wa jimbo hilo wakati juhudi za uokoaji zikiwa bado zinaendelea.
Akizungumza na waandishi wa habari gavana wa Texas, Greg Abbott ametangaza rasmi hali ya maafa, akilitaja tukio hilo kuwa ni “janga lisilo la kawaida.
Mafuriko hayo yalitokea baada ya kukatika kwa kingo za Mto Guadalupe baada ya mvua kubwa kunyesha katika jimbo hilo siku ya Ijumaa wiki iliyopita.
Wakati hayo yakiendelea, Rais wa Marekani Donald Trump amesema huenda akalitembelea eneo hilo lilokubwa na maafa siku ya Ijumaa ya wiki hii.