JangaNigeria
Mafuriko yasababisha vifo vya watu 200 Nigeria
3 Juni 2025Matangazo
Kamishna wa masuala ya kibinadamu wa jimbo la Niger Ahmad Suleiman ameviambia vituo vya televisheni hii leo, huku mamia ya watu wengine wakiwa hawajulikani walipo, na kuna wasiwasi kwamba wamefariki.
Amesema bado wanaendelea kuwatafuta wahanga hao, ingawa hawana uhakika wa kuwapata.
Mji wa Mokwa ulikumbwa na mafuriko mabaya zaidi siku ya Alhamisi kutokana na mvua zilizonyesha usiku kucha, huku zaidi ya nyumba 250 zikiharibiwa na mafuriko.
Mabadiliko ya hali ya hewa yametajwa kusababisha hali hiyo nchini Nigeria, ingawa wakaazi wa Mokwa wamesema sababu za kibinadamu pia zimechangia.