Idadi ya waliofariki katika maandamano Kenya yafikia 38
12 Julai 2025Matangazo
Katika taarifa, KNCHR ilithibitisha kuongezeka kwa idadi hiyo ya waliouawa na kusema kuwa takriban watu wengine 130 walijeruhiwa katika maandamano hayo ya Jumatatu.
Tume hiyo imeongeza kuwa huku ukishuhudia vifo vya watu wanane, mji wa Kiambu ndio uliokuwa na idadi kubwa zaidi ya waathiriwa, kufuatiwa na mji mkuu Nairobi na Kajiado katika eneo la kusini ambayo yote ilishuhudia vifo sita.
Rais wa Kenya aonya dhidi ya jaribio la 'kuipindua ' serikali
Awali, KNHCR, iliripoti kuuawa kwa watu 31.
Idadi hiyo iliyoongezeka inaifanya Jumatatu kuwa siku mbaya zaidi ya maandamano tangu kuanza kwa maandamano yanayoongozwa na vijana dhidi ya serikali ya Rais William Ruto, ambayo yametikisa nchi hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja.