Idadi ya visa vya Ebola nchini Uganda yafikia 9
11 Februari 2025Matangazo
Taarifa ya wizara ya afya ya nchi hiyo imesema wagonjwa 7 kati ya 9 wanapatiwa matibabu kwenye hospitali moja ya mji mkuu, Kampala na mgonjwa mwingine amelazwa katika hospitali ya mji wa mashariki wa Mbale karibu na mpaka na Kenya. Mtu mmoja ndiye amekufa tangu janga hilo lilipozuka. Kulingana na wizara ya afya, wagonjwa wote wanane wako kwenye hali nzuri, na watu 265 waliowahi kukutana na wagonjwa hao wamewekwa karantini. Hivi sasa Uganda inatoa chanjo ya majaribio dhidi ya kirusi cha Ebola klichoanzia Sudan. Chanjo hiyo iliidhinishwa kutumika kwa muda na Shirika la Afya Duniani WHO, mwezi uliopita.