MigogoroAsia
Idadi ya vifo yaongezeka kufuatia mapigano Cambodia
26 Julai 2025Matangazo
Zaidi ya watu 35,000 wamelazimika kukimbia makazi yao. Kulingana na msemaji wa wizara hiyo, wanajeshi watano na raia wanane wamepoteza maisha. Mapigano makali yamekuwa yakiendelea kati ya nchi hizo mbili jirani tangu tarehe 24 Julai, kutokana na mzozo wa muda mrefu wa mpaka.
Kwa upande wake, Thailand imetangaza hali ya hatari ya kijeshi katika wilaya nane zinazopakana na Cambodia. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya mkutano wa dharura Ijumaa jioni kujadili mapigano ya mpakani.
Wakati huo huo, Malaysia, ambayo ndiyo mwenyekiti wa jumuiya ya kikanda ya ASEAN inayozijumuisha nchi hizo mbili, imetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano na kujitolea kuwa mpatanishi. Pande zote mbili zinalaumiana kwa kuchochea ghasia hizo.